Kauli hiyo ni wito kwa wanachama wote wa shirika hilo kuunga mkono juhudi hiyo kama ni "kazi ya dharura". Bi. Bokova alisema, amehuzunishwa na hali ya uharibifu mkubwa wa urithi wa utamduni wa Mali, ambayo imetokea katika miezi kadhaa iliyopita.
Amesisitiza kuwa shirika la UNESCO litafanya juhudi ya kushirikiana na watu wa Mali ili kukarabati upya urithi muhimu wa utamaduni nchini humo, ikiwemo ukarabati wa kaburi la Timbuktu na kaburi la Askia lililoko huko Gao.